CESC FABREGAS KUZOMEWA UWANJA WA EMIRATES JUMAPILI HII?…HAYA NI MAWAZO YA WENGER.


CESC FABREGAS KUZOMEWA UWANJA WA EMIRATES JUMAPILI HII?…HAYA NI MAWAZO YA WENGER.

cc

Hii itakua mara ya kwanza kwa Cesc Fabregas kwenda kwenye uwanja wa Emirates na kucheza against timu yake ya zamani kwenye EPL ambayo ni Arsenal. Jumapili hii kwenye EPL kuna mechi kati ya Chelsea na Arsenal ambapo Cesc Fabregas anatengemewa kucheza mechi hii.

Kuna uwezekano wa Cesc Fabregas kuzomewa kwenye mechi hii na mashabiki wa Arsenal lakini kocha Arsenal Wenger ana mawazo tofauti. Kocha Wenger amesema kwamba mashabiki wa Arsenal waendelee kumheshimu Cesc Fabregas licha ya kuondoka Arsenal akiwa bado ni mchezaji muhimu. Pia Wenger ameongezea kwamba bado anajilaumu kwa kumruhusu Cesc Fabregas kuondoka Arsenal.

Kama wewe ni shabiki wa Arsenal na ungekua uwanja wa Emirates jumapili hii…ungemzomea au ungekausha?

 



Comments