Taarifa mpya            kutoka katika vyanzo vya habari nchini Italia na Ufaransa ni            juu ya wawakilishi wa mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay,            Edinson Cavani kukutana na menejimenti ya Paris Saint-Germain.
        Kwamba lengo            la mkutano huo ni kujadili ofa kutoka Juventus, Manchester            United na Atletico Madrid zinazotaka huduma ya staa huyo wa            zamani wa Napoli mwenye umri wa miaka 28.
        Habari zaidi            zinapasha kuwa kama PSG itaamua kumwachia Cavani kuondoka,            basi atakwenda Juventus ili kuirahisishia klabu hiyo ya            Ufaransa kupata saini ya Paul Pogba.
        
Comments
Post a Comment