CARLO ANCELOTTI ASEMA UBINGWA WA LA LIGA BADO UKO WAZI KWA REAL MADRID


CARLO ANCELOTTI ASEMA UBINGWA WA LA LIGA BADO UKO WAZI KWA REAL MADRID
Carlo Ancelotti's Real            Madrid hope to become the first club to defend the Champions            League trophy
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti anaamini mbio za ubingwa wa La Liga zitakwenda hadi mwisho baada ya timu zote mbili za juu – pamoja na Barcelona iliyo kileleni kushinda mechi zao ngumu Jumamosi.
Vijana wa Ancelotti walishinda 3-1 dhidi ya Malaga nyumbani Estadio Santiago Bernabeu huku Barcelona nao wakiwachapa Valencia 2-0 na kuendelea kuwa juu kwa tofauti ya pointi mbili.
"Natarajia ubingwa utaamuliwa katika mechi ya mwisho," alisema Ancelotti. ""Tunataka kubaki hai katika La Liga, na timu mbili (Barca na Madrid) zina michezo migumu, kwa sababu sasa kuna mambo mengi katika kucheza."


Comments