Real Madrid inatarajiwa kushuka dimbani leo usiku kuwakaribisha wapinzani wao wa mji mmoja, Atletico Madrid katika marudiano ya robo fainali ya Champions League bila wachezaji wake wanne muhimu, lakini kwa Carlo Ancelotti hilo si tatizo.
"Sisi ni kikosi bora duniani," anasema Ancelotti ambaye atawakosa Modric, Bale, Benzema na Marcelo walio majeruhi.
Akiwatoa hofu wachezaji wake kutokana na kukosekana nyota hao kabla ya mazoezi yao ya Jumatatu katika Uwanja wa Valdebebas, Ancelotti alisema: "Hakuna matatizo Real Madrid… Kuna ufumbuzi pekee, na kila mmoja miongoni mwenu ninayemuona hapa ni mkali."
Akizungumza baadaye na Radio Anch'io Sport, Ancelotti alisema hana woga kutokana na kuwapo majeruhi, na kwamba atapata ufumbuzi.
Kwa mujibu wa mtandao wa Marca, Ancelotti anatarajiwa kupanga kikosi chake hivi: Casillas, Carvajal, Ramos, Varane, Coentrao, Kroos, Illarra, Isco, James, Ronaldo na Javier 'Chicharito' Hernández.
Kwa mujibu wa mtandao wa Marca, Ancelotti anatarajiwa kupanga kikosi chake hivi: Casillas, Carvajal, Ramos, Varane, Coentrao, Kroos, Illarra, Isco, James, Ronaldo na Javier 'Chicharito' Hernández.
Comments
Post a Comment