Ikitoka nyumba 3-1 kufuatia kipigo walichokipata ugenini wiki iliyopita, Bayern ikaibuka na kidedea uwanja wa nyumbani baada ya kuvuna ushindi mkubwa wa 6-1 dhidi ya Porto.
Porto ilishindwa kabisa kulinda hazina ya ushindi wa 3-1 iliokuwa nao mkononi na kujikuta ikibugizwa 5-0 hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Kwa ushindi huo, Bayern inatinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya bao 7-4.
Mabao ya Bayern yalifungwa na Thiago, Jerome Boateng,Thomas Muller, Xabi Alonso na Robert Lewandowski aliyefunga mara mbili. Bao pekee la Porto lilifungwa na Jackson Martinez.
Bayern Munich XI: Neuer, Rafinha, Boateng, Badstuber, Bernat, Lahm, Alonso, Thiago, Muller, Gotze, Lewandowski.
Bayern subs: Reina, Dante, Pizarro, Gaudino, Rode, Weiser, Schweinsteiger.
Porto XI: Fabiano, Reyes, Maicon, Marcano, Indi, Herrera, Casemiro, Torres, Quaresma, Martinez, Brahimi.
Comments
Post a Comment