BARCELONA YAENDELEA KUGAWA DOZI KUBWA KUBWA, GATAFE YABUGIZWA 6-0 ...Ni Messi, Neymar na Suarez kama kawaida yao
Kwa wale waliokuwa wakidhani utatu wa washambuliaji balaa Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar hautafanya kazi Barcelona, basi imekula kwao, wanaume wanacheka na nyavu kila mechi.
Barcelona imezidi kujitanua kileleni mwa La Liga baada ya kuichapa Getafe 6-0 huku Messi na Suarez wakifunga mara mbili kila mmoja wakati Neymar akifunga mara moja.
Mwanzoni mwa msimu huu baadhi ya wachambuzi walibashiri kuwa washambuliaji hao watatu hawawezi kucheza kwa pamoja na kutengeneza mafanikio, lakini sasa mambo yamekuwa ni kinyume.
Bao lingine la Barcelona katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Camp Nou, lilifungwa na kiungo mkongwe Xavi.
Neymar akishangilia na Lionel Messi baada ya kuifungia Barcelona bao la tatu kwenye uwanja wa Nou Camp Jumanne usiku.
Ni wazi kuwa Barclona sasa kasi yao ya kuelekea kutwaa taji la La Liga, haizuiliki. Wamesimama kileleni wakiwa mbele kwa pointi tano safi.
Barcelona sasa imetupia wavuni magoli 153 msimu huu. Messi akiwa na 49, Neymar 32 and Suarez 21. Jumla ya magoli ya wakali hap watatu inafikia 102 wakivunja rekodi ya magoli 100 yaliyofungwa Samuel Eto'o, Thierry Henry naMessi katika msimu wa 2008-09.
Washambuliaji tishio wa Barcelona Messi, Neymar and Luis Suarez wakiwa na furaha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya ushindi wa 6-0.
Kwa picha zaidi nenda: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3059647/Barcelona-6-0-Getafe-Lionel-Messi-Neymar-Luis-Suarez-pass-100-goals-season-Luis-Enrique-s-five-points-clear-Real-Madrid.html#ixzz3YdvwJivw
Comments
Post a Comment