Baada ya ku-launch mtandao wa simu ambao unatumia jina lake 'Eto'o Telecom' huko kwao Cameroon, Samuel Eto'o ameendelea kufunguka zaidi kwenye uwekezaji mwingine.
Kama unamfatilia sana Eto'o ni mtu ambae anapenda sana kutupia kama watoto wa mjini wasemavyo. Mara kadhaa huwa anavaa nguo kutoka kwa fashion designer wakubwa duniani hasa Ulaya.
Kinachofuata ni ku-launch brand mpya kwenye fashion ambayo itatumia jina la 'Samuel Eto'o 9' na nguo hizo zitakua hasa kwa wanaume. Hivi sasa toleo la majaribio limeshafanyika na nguo hizo zinatengenezwa huko Uturuki, baada ya kutoa nguo za majaribio zimefanya vizuri sokoni.
Gabriel Pascal Nlend fashion designer kutoka Cameroon ambae anasimamia project nzima amesea hivi, "Project hii ni kutambua mafanikio na mchango wa Samuel Eto'o kwenye mpira kwake yeye binafsi na kwa bara la Africa.Kununua hizi product ni kama kusema asante kwa kufurahia kila moment ambayo Eto'o aliichangia akiwa uwanjani."
Brand Eto'o imeingia kwenye mavazi na labda itafika hadi Tanzania kwasababu bei zake zitakua affordable kwa Africa.
Comments
Post a Comment