Arsenal imeripotiwa kuwa kwenye harakati za kufanya uhamisho wa kushtua utakaompeleka Emirates kocha Jurgen Klopp kuchukua nafasi ya Arsene Wenger kiangazi hiki.
Klopp, ambaye ni mmoja wa makocha wanaowindwa zaidi kwa sasa, anajiandaa kuwa huru wakati atakapoondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu.
Manchester City inatajwa kuwa katika nafasi kubwa ya kumnasa kocha huyo, lakini gazeti la Ujerumani la Kicker limeripoti kuwa Arsernal iko 'siriaz' kutaka huduma yake.
Gazeti hilo lililojipatia umaarufu kwa kuibuka na stori 'exclusives' ambazo mara nyingi ubeba uhalisia limesema katika taarifa yake kuwa Arsenal ina nia ya kweli ya kutaka kumfanya Klopp mbadala wa Wenger.
Utakuwa uhamisho wa kushangaza kutokana na ukweli kuwa Wenger anafurahia msimu mzuri, lakini Kicker linaonekana kuwa na uhakika na ilichokiandika.
Comments
Post a Comment