ARSENAL YAKARIBIA KUMNASA HECTOR MORENO WA ESPANYOL



ARSENAL YAKARIBIA KUMNASA HECTOR MORENO WA ESPANYOL

Arsenal inakaribia kushinda mbio za kumuwania beki wa Espanyol ya Hispania, Hector Moreno baada ya nyota huyo kuelezea nia yake ya kutaka kujiunga na klabu hiyo.
Tottenham na Manchester United zote zinamuwania beki huyo wa kati, lakini kwa mujibu wa gazeti la The Express chaguo lake la kwanza ni kuungana na Arsene Wenger ndani ya Emirates.
Ripoti zinasema Moreno amemwambia wakala wake kuweka mipango sawa aweze kuhamia kaskazini mwa London kiangazi hiki baada ya kuivutia Arsenal kwa kiwango chake msimu huu.
Inaaminika kwamba ofa ya karibu pauni milioni 15 itatosha kuishawishi Espanyol kumwachia.


Comments