Jose Mourinho ameanzisha tena vita ya maneno na Arsenal akisema kukaa miaka 11 bila kombe ndiko 'kunaboa".
John Terry akiwa kwenye kiwango cha juu zaidi kuwahi kutokea, kwa mujibu wa Mourinho aliiongoza Chelsea kupata suluhu Emirates na kuukaribia ubingwa wa ligi kuu England.
Mashabiki wa Arsena walikuwa wanawazomea Chelsea kwa staili yao ya kujihami wakidai inaboa.: 'Boring, boring".
Mawazo ya mashabiki yaliendana na Arsene Wenger aliyedai Chelsea walienda Emirates kujilinda tu na si kucheza mpira, lakini Mourinho aliyeanza mechi bila kuwa na mshambuliaji wa kati wa wazi amejibu mapigo akisema kitendo cha Arsenal kukaa miaka 11 bila ubingwa wa ligi kuu ndiko kunaboa.
"Inaboa, nadhani ni miaka 10 bila ubingwa. Hii inaboa" amesema Mreno huyo.
"Unaishangilia timu na unasubiri, unasubiri, unasubiri kwa miaka mingi bila kombe, huko ndiko kunaboa"
Comments
Post a Comment