ARSENAL SASA YAHUSISHWA NA IKER CASILLAS



ARSENAL SASA YAHUSISHWA NA IKER CASILLAS

Arsenal imepata msukumo mkubwa katika harakati zake za kukamilisha uhamisho wa kushtua wa kipa wa Real Madrid, Iker Casillas baada ya kubainika kuwa miamba hiyo ya Hispania inajaribu kumshawishi aondoke Santiago Bernabeu.
Gunners ina nia ya kumsajili kipa huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 33 na inaweza kutimiza lengo iwapo Mhispania huyo atatangaza kuondoka Madrid.
Casillas ana mkataba hadi 2017 na kwamba anataka heshima katika klabu yake, lakini kwa mujibu wa kituo cha redio cha Onda Cero, Madrid iko tayari kumlipa ili aondoke na kujiunga na Arsenal au Liverpool.
Arsene Wenger anafuatilia kwa karibu hali ya mambo inavyokwenda Madrid.


Comments