Arsenal imejipanga kulipa pauni milioni            10.7 kwa ajili ya uhamisho wa beki anayepanda wa klabu ya            Torino ya Italia, Matteo Darmian.
        Kwa mujibu wa gazeti la Forza, staa huyo            wa zamani wa Palermo mwenye umri wa miaka 25 aliitamanisha            zaidi Arsenal baada ya kufunga bao moja na kupika jingine            katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Juventus.
        Hata hivyo, Arsene Wenger anakabiliwa na            upinzani kutoka kwa miamba ya Ulaya, Barcelona na Bayern            Munich ambazo pia zinatamani huduma ya beki huyo aliyepanda            thamani kutokana na kiwango chake bora msimu huu.
        
Comments
Post a Comment