Alichokisema Msuva kuhusu goli lake linalofanana na la Van Persie…



Alichokisema Msuva kuhusu goli lake linalofanana na la Van Persie…

NgassanaMsuva

SIMON Happygod Msuva amesema anajisikia furaha kuchukua ubingwa huku goli lake la kichwa alilofunga kwa kichwa dhidi ya Ruvu Shooting likijadiliwa mno kwenye mitandao ya kijamii na kufananishwa na alilofunga mshambuliaji wa Manchester United na Uholanzi, Robin van Persie kwenye fainali za kombe la dunia mwaka jana nchini Brazil.

"Watu wanasema nilifunga kama Robin Van Persie, wanajadili sana kwenye mitandao, haya ni mafanikio kwangu, juhudi ndio siri ya mafanikio" Amesema Msuva.

Winga huyo anayeongoza orodha ya wafungaji akiwa amefumania nyavu mara 17 msimu huu akifuatiwa na Amissi Tambwe mwenye magoli 14 ameongeza kuwa ubingwa waliopata anafurahi kuchangia kwa kiasi kikubwa na ataendelea kufanya vizuri.

"Huu ni mwanzo tu, kila siku najifunza na kupunguza makosa, tuna kocha mzuri, tunaamini tutafanya vizuri zaidi siku zijazo tukianzia na mechi ijayo dhidi ya Etoile du sahel". Amesema Msuva.



Comments