Yaya Toure amewatosa wachezaji wenzake wa Manchester City baada kushindwa kumtaja hata mmoja katika kikosi chake bora cha wachezaji 11.
Kiungo huyo akaamua kuwaweka kando nyota wa City kama Sergio Aguero, David Silva na Vincent Kompany na kuwataja wachezaji wenzake wa zamani Gerard Pique, Dani Alves, Andres Iniesta, Xavi na Lionel Messi aliokipiga nao ndani ya Barcelona.
Na katika kutia chumvi kwenye kidonda, Toure akawataja wachezaji wanne Iker Casillas, Sergio Ramos, Cristiano Ronaldo na James Rodriguez kutoka Real Madirid ambao ni wahasimu wakubwa wa Barcelona.
Kikosi kamili cha Yaya Toure ni: Casillas, Ramos, Pique, Hummels; Dani Alves, Iniesta, Xavi, Schweinsteiger, James Rodriguez; Ronaldo, Messi.
Comments
Post a Comment