Bendi ya muziki wa kizazi inayotesa ndani na nje ya mipaka ya Bongo, Yamoto Band watafanya vitu vyao Mtwara mjini tarehe 21 mwezi huu.
Mkubwa Fella ameiambia Saluti5 kuwa vijana wake watafanya onyesho maalum katika ukumbi wa Makonde Beach na kuachia nyimbo zao mpya kabisa sambamba na zile za zamani zinazoendelea kutesa sokoni.
Fella amesema hiyo ni zawadi nzuri kwa wakazi wa Mtwara baada ya ziara ya mafanikio ya Yamoto Band ndani ya Uingereza.
Comments
Post a Comment