Wenger atamani kucheza Europa ligi


Wenger atamani kucheza Europa ligi

WENGERNa Augustino Mabalwe,Dar es salaam

Baada ya timu ya Arsenal kutolewa katika michuano ya klabu bingwa ulaya na klabu ya Monaco kocha wa washika bunduki hao Arsene Wenger amesema timu yake itafanya vizuri kama itashiriki michuano ya Europa ligi kuliko kuendelea katika mashindano haya ya klabu bingwa.

Licha ya ushindi wa jana wa 2-0 katika uwanja Louis ll kikosi cha mfaransa huyo kilitolewa kwa sheria ya goli la ugenini na ikawa ni mara ya 5 mfululizo timu hiyo kutoka katika hatua ya 16 bora kwenye michuano hiyo.

Klabu ya Arsenal imekuwa ikitolewa katika hatua hii kufuatia kushindwa kutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani na hivyo kujikuta wanarudia makosa yaleyake kila msimu. "Tulionesha kiwango kizuri, tuliumiliki mchezo lakini kipindi cha pili tulikosa umakini. Nimesikitishwa sana kutolewa katika hatua hii ila nitakumbuka makubwa katika mechi hii. " alisema Wenger.

Timu hiyo sasa inakibarua kizito cha kupambana na klabu ya Reading katika hatua ya nusu fainali kombe la FA katika dimba la Wembley lakini pia inahaha kusaka nafasi ya kucheza michuano ya klabu bingwa msimu ujao kufuatia ushindani wa ligi hiyo kuzidi kuongezeka kila siku.



Comments