Wanyama kutimkia Arsenal?



Wanyama kutimkia Arsenal?

Victor WanyamaNa George Mganga "Amplifaya"

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga
kumnunua kiungo wa kati wa Southampton
Mkenya Victor Wanyama na mshambuliaji wa
Anderlecht Aleksandr Mitrovic kulingana na
gazeti la the Sun nchini Uingereza.

Wenger amejiandaa kutoa kitita cha pauni
millioni 30 kwa wachezaji hao wawili,huku
Wanyama akigharimu kitita cha pauni millioni 20
naye mshambuliaji huyo wa Anderlecht Mitrovic
akigharimu pauni millioni 10.

Inaaminika kuwa Wanyama ataondoka katika
kilabu ya Southampton iwapo atachukuliwa na
kilabu kikubwa huku naye Mitrovic akiwa
amekuwa akifuatiliwa na waajiri wa Arsenal
katika kipindi cha wiki chache zilizopotea.
Mitrovic amekuwa akifananishwa na Didier
Drogba kutokana na mchezo wake.



Comments