Vermaelen arejea mazoezini



Vermaelen arejea mazoezini

26FBF61A00000578-3011185-The_former_Arsenal_man_right_in_training_on_Wednesday_is_yet_to_-a-24_1427302371884Na Augustino Mabalwe,Dar es salaam

Beki wa klabu ya Barcelona Thomas Vermaelen jana amerejea mazoezini baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu akiuguza majeraha.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mapema mwezi desemba mwaka jana alifanyiwa upasuaji kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja aliyoyapata kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Brazil.

Vermaelen,29, hajawahi kuichezea Barcelona hata mechi moja tangu asajiliwe msimu huu akitokea katika klabu ya Arsenal.

Mchezaji huyo alijiunga katika mazoezi ya timu hiyo hapo jana pamoja wenzake ambao hawajaenda katika majukumu ya timu ya taifa.

Kikosi hicho kilichoibuka na ushindi katika mechi ya El Classico jumapili iliyopita, kinataraji kushuka dimbani kukipiga dhidi ya Celta Vigo mara baada ya michezo ya kimataifa kumalizika.



Comments