Uganda na Tanzania kuchuana mwishoni mwa wiki hii “Kriketi”


Uganda na Tanzania kuchuana mwishoni mwa wiki hii "Kriketi"

Timu ya Kriketi ya TanzaniaNa George Mganga 'Amplifaya'

Tanzania imepangwa kucheza na Uganda katika
mechi ya ufunguzi ya michuano ya Afrika Ligi
Daraja la kwanza itakayofanyika nchini Afrika ya
Kusini katika mji wa Benoni mwishoni mwa wiki
hii.

Chama cha Kriketi nchini Tanzania kimeteua
timu ya taifa kwa ajili ya michuano hiyo na tayari
timu hiyo imeondoka Tanzania kuelekea Afrika
ya Kusini.

Nahodha wa Tanzania, Hamisi Abdallah
amesema Uganda sio timu ngeni na
wanaichukulia mechi yao kwa umuhimu
mkubwa.Nchi nyingine zinazotegemewa kushiriki
michuano hiyo ni Kenya, Namibia, Botswana na
Ghana.

Abdallah anaendelea kuwa nahodha wa timu hiyo
kwa zaidi ya muongo mmoja (miaka 10) akiwa
na uzoefu wa kutosha wa michuano ya
kimataifa, huku akiwa na rekodi ya kucheza
kriketi nchini Uingereza katika klabu ya Watford
Town.

Wachezaji wengine waliochaguliwa katika timu
hiyo ni Abhik Patwa, akiwa na rekodi ya kufunga
nusu century ( runs 50) katika michuano iliyopita
ambapo Nigeria na Ghana waliibuka vinara.

Wachezaji wengine ni Yakesh Patel, Ally Mpeka,
Arshan Jassani, Riziki Kiseto, Zamoyoni
Jabeneke,Harsheed Chohan, Issa Kikasi,Kassim
Nassoro, Arun Dagar, Khalil Rehemtullah, Martin
Mwarabu na Rahil Amarshi.



Comments