Thiery Henry na imani kwa Arsenal kumaliza ukame wa mataji


Thiery Henry na imani kwa Arsenal kumaliza ukame wa mataji

27060BBE00000578-0-image-a-1_1427451680732Na George Mganga "Amplifaya"

Akiwa kama mchezaji mstaafu wa timu ya Arsenal Thiery Henry amejaribu kuweka utofauti wa vilabu viwili, moja ikiwa ni kilabu mama kwake halikadhalika Liverpool.

Mchezaji huyo amekuwa na matarajio makubwa zaidi ndani ya kilabu yake ya zamani kuwa haitokuwa na ukame wa mataji katika siku za usoni hasa katika ligi kuu ya Uingereza kama wengi ambavyo hawaamini ukitofautisha na Liverpool.

Anasema kuwa Liverpool tokea mwaka 1990 haijatwaa kombe la Uingereza la ligi na tokea wakati huo imekuwa ikichezea nafasi ya kumi bora na imekosekana katika ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa miaka kadhaa sasa ukiachilia kilabu yake mama ambayo bado imekuwa ikishiriki kila msimu.

"Ningekuambia kuwa mwaka 1990 Liverpool haitoweza kushinda kombe la ligi kwa miaka 25 ijayo ungeniona mwendawazimu" "sitaki kuona hili jambo likitokea katika timu ya Arsenal" alitamka hayo wakati anaongea na waandishi wa habari.

Katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza Arsenal wapo nafasi ya Tatu na pointi zao 60 hivi sasa wakiwa na tofauti ya point 7 na Chelsea ambao wanaongoza ligi hiyo.

Utofauti wa gepu la Arsenal na Chelsea kulifikia kwasasa sio jambo la kawaida wala la kupuuzia haswa wakati huu wa mwisho ambapo ligi hiyo inaelekea ukingoni, Henry anaamini kuwa wachezaji wale wale wa siku zote ndani ya timu hiyo ndiyo watakaoifikisha timu hiyo mbali na kutwaa ndoo siku zijazo za usoni.

Katika michuano ya kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya Arsenal ilishindwa kuendelea mara baada ya kutolewa na Monaco katika raundi ya 16 bora na hii ni Mara baada ya kushindwa kutumia nafasi katika uwanja wao wa nyumbani kuruhusu goli 3-1 na kushinda ugenini kwa goli 2-0 kitu ambacho hakikusaidia katika aggregate.24193A7400000578-0-image-a-4_1427451893141

Juu ya hayo aliweka wazi pia kuwa timu yake ipo vizuri lakini ilipoteza pointi mwanzoni mwa msimu lakini akiamini uwezekano wa kubeba kombe utakuwepo kwa misimu ijayo.

"Nadhani kwa miaka ijayo uwezo wa kutwaa kombe la ligi utakuwepo" alisema.

Henry alikuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal wakati inaitwaa taji la ligi kuu ya Uingereza msimu wa mwaka 2003-2004 msimu ambao Arsene Wenger alisema rekodi ya kumaliza ligi akiwa hajafungwa mechi yoyote.

Henry aliamua kupumzika kusakata kambumbu mnamo mwezi wa 12 mwaka jana ikiwa ni moja ya ndiyo zake za mafanikio na ndipo alipoamua kujiingiiza katika majukumu mengine, kumbuka pia uwepo wake ndani ya Arsenal uliisaidia timu hiyo kupata mafunzo katika academy ya washika bunduki hao.

Mchezaji huyo alisema kwasasa anataka kwenda kukamilisha malengo yake mengine ya ualimu wa wa mpira pia akiwa na ndiyo za kuwa mchambuzi wa mpira wa miguu katika kituo cha soka cha Sky Sports na haya aliyasema wakati akizungumza na Shaffih Dauda mchambuzi wa soka mapema baada ya kutangaza mshindi wa Ballon D'or huko Zurich.26F4B85D00000578-0-image-a-2_1427451731013



Comments