Nichukue fursa hii kuwapa pole baadhi ya timu za ligi kuu ya Tanzania bara ambazo zinaathiriwa kwa kiasi kikubwa na panga pangua ya ratiba ya ligi.
Ligi imekuwa haieleweki kwa sasa, unaamka J/tatu ukiwa na ratiba ya kucheza J/tano lakini bado unakuwa huna uhakika kama utacheza au mechi itaahirishwa?
Hiyo ndiyo ligi tunayokwenda nayo hivi sasa utadhani ni yale makombe ya mbuzi ya mchangani ambayo mechi inaweza ikasogezwa mbele bila ya sababu za kimsingi, ni maamuzi tu ya mwenye kombe ndo yanafanya kazi.
Uongozi wa Jamal Malinzi ulipigiwa chapuo sana na wadau wa michezo nchini wakati wa uchaguzi wakini huenda ukaleta mabadiliko katika soka letu, lakini cha kushangaza uongozi huu leo ratiba tu ya ligi yenye timu 14 inawasumbua katika upangaji, je hayo majukumu mengine makubwa yanatekelezwa kwa ufasaha kweli?
Napata tabu kuelewa, hivi Tff hawajui umbali wa kutoka Dar es salaam hadi Mbeya? Mpaka wawatoe Prison ambao walikuwepo Dar wakijua wanamechi wakawaambia warudi Mbeya wakacheze na Yanga, hii ni ajabu, wakati hilo halijasahaulika wakaibuka tena na kuwataka Mgambo ya Tanga ambao tayari walishafika Mbeya kwa ajili ya Mechi warudi Tanga kucheza na Azam, kama ingekuwa sio kuomba kwa timu ya Yanga kuahirishiwa mechi yake ya J/tano jambo ambalo limewafanya Tff waone aibu na kuahirisha mechi zote za J/tano basi nina uhakika Mgambo wangelazimishwa kurudi Tanga ingawa tumewasikia viongozi wa Mgambo wakigomea suala hilo la kurudi kuchea Tanga.
Nimejiuliza saba, hivi hawa wazungu mbona hatusikii ratiba zao kupanguliwa namna hii? mfano Uingereza ligi ina timu 20, kuna timu zinacheza klabu bingwa ulaya, kuna kombe la ligi, kuna kombe la FA, kuna kombe la Carling lakini hutasikia ratiba kupanguliwa na zipo timu ambazo zinashiriki makombe yote niliyoyataja.
Ligi kuu ya Tanzania ina timu 14, hakuna mashindano mengine yanayoandaliwa na Tff, lakini bado ratiba hiyo ndogo tu inawashinda.
Utasikia "mechi za tarehe fulani zinasogezwa mbele kupisha mechi ya kirafiki ya timu yaifa ambayo ipo katika kalenda ya Fifa", hapa ndo huwa nachoka sana, hivi wakati wanapanga ratiba huwa hawazingatii kalenda ya Fifa? Mbona kwa wenzetu hayatokei haya?
Je! Tff wanataka kutuaminisha kuwa wazungu wametuacha mbali sana kiakili?
Au ni matatizo yao wenyewe tu kutokuwa makini na kazi zao?.
Tusubiri tuone ratiba itakavyopanguliwa tena.
Ni halali yako kushare nami mawazo yako, maoni, ushauri kuhusiana na soka kwa ujumla mtu wangu kupitia hii namba
0688665508
Comments
Post a Comment