Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga, amesema hana mpango wa kujitosa kuwania nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Tenga, rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ameyasema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habri kwenye ofisi za makao makuu ya TFF zilizopo Karume jijini hapa.
Amesema kuwa kanuni za sasa za CAF zinambana kufikiria kushika nafasi hiyo kubwa ya uongozi wa soka barani.
"Ukiwa mwanafamilia wa CAF inakuwa ngumu kufikiria kuanza kuwashawishi wajumbne wakuchague kushika nafasiu kubwa kama hiyo ilhali kuna mwenzenu anaishikilia," Tenga amesema.
"Unapofanya hivyo, ni lazima utaangusha timu. Wenzako wanafikiria mipango ya maaendeleo, wewe unawaza namna ya kuingia madarakani."
Tenga, nahodha wa zamani wa Taifa Stars, kwa sasa ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na kanuni za uchaguzi za shirikisho hilo zinatamka wazi kwamba mgombea wa nafasi ya urais wa CAF ni lazima atoke mionongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo
Comments
Post a Comment