TELELA, MKUDE? TAIFA STARS NA NGAZI YA KUFIKIRIKA



TELELA, MKUDE? TAIFA STARS NA NGAZI YA KUFIKIRIKA

JONAS MKUDE NA MESSINa, Nicasius Coutinho Suso

Maandalizi ni msingi wa mafanikio ya jambo lolote lile, Binadamu hutegemea hili katika kuweka mambo sawa na kwa muda mrefu, Ndivyo maisha yalivyo,  unajiandaa ili uje kuwa bora katika kile unachokifanya,  Hakuna njia fupi katika maisha,  hata soka lipo hapa,  na michezo ipo hapa. Hakuna anayeweza kuamka na kujikuta juu ya ngazi kama hakuwahi fanya maamuzi ya kuipanda.

Umekiona kikosi cha taifa, Taifa Stars? Ni Kikosi bora kabisa lakini sio kwa leo au kwa wakati huu,  ni kikosi bora kilichotakiwa kuwepo miaka mitano nyuma.

Wakati Aggrey Moris,  Kiemba,  Kazimoto Wana uwezo wa kukimbia kwa jitihada na moyo huo huo miaka mitatu mfululizo katika ngazi zote za klabu na taifa.

Sio kikosi bora kwa leo wakati wanatizama pensheni zao klabuni na umakini kulinda afya zao. Lakini unajiuliza pia kocha ameita kwa sababu zipi?  Kuifunga Malawi?  Kupanda katika orodha ya Fifa? Au kuiandaa timu kwa michuano ya baadae? Nina uhakika jibu linaweza lisitoke humu kwenye niliyoyasema.

Katika Afcon ya mwaka 2015 Januari,  Congo Brazzaville walikuwa na kikosi chenye wastani mdogo zaidi wa miaka 23.3. Hawa hawakushiriki Afcon ya mwaka 2013 achilia mbali 2012, 2010 na kuendelea. Maana yake kwa wastani wakati wa Afcon zilizopita walikuwa na kikosi kilichokuwa na miaka 21, na pia maana yake Wana kikosi chenye uwezo wa kufika Afcon inayofuata 2017, kombe la dunia 2018 mpaka lile la 2022 wakiwa bado na nguvu kabisa usiwaze mabadiliko wanayoweza kuyafanya.congo_

  Wale South Africa walikuwa na 24, Unaona nini hapa,  kuwa soka Sasa limebadilika, soka lipo katika kuwekeza kwa vijana kuliko watu wazima, Hawa vijana ndio wakuliweka taifa mahala salama, Hawa ndio wanaoweza kutupa furaha mbele, Lakini sisi hatuwazi Hilo.

Akicheza Isihaka akajifunga mashabiki na vyombo vya habari vitahoji kwanini hachezi Cannavaro, Chanongo tutauliza alikosaje pale bora awepo Kiemba, Kibaya zaidi tunawaza kuwapa hata uraia Coutinho na Tcheche.

Unasubiri Mkude apate majeraha ndo atumike,  unashindwaje kumpa kipaumbele Mandawa katika wakati huu achilia mbali Telela, Kessy na Tshabalala, Tunataka kuishi kiuongo uongo katika maisha yaliyojaa ukweli ndani yake, mwisho wa siku uwanjani Dunia inatutenga peke yetu.shabalala

Bahati mbaya Sana hata katika nyanja nyingine za kitaifa tunasema vijana ndo taifa la kesho, Tunaamini katika vijana tukiwa katika maandishi lakini machoni na mioyoni tunasema tofauti,  Sina nia ya kuwaza au kudadavua utashi wa viongozi wetu wa soka lakini unajiuliza huu ndo mpango endelevu wa soka letu? Hii ndo sababu ya kuleta kocha wa kigeni?

Wa nini Sasa,  kumsimamia Nadir,  Kiemba, Kazimoto, Munishi uwanjani?  Au kuwajenga akina Telela kiuwezo?  Kama tumemleta kusimamia Hao basi Julio anaiweza hiyo kazi,  lakini kama tumemleta kujenga vijana kiuwezo kwa matumaini na matokeo bora basi Hapana shaka Kuna tatizo hapa,  kama sio kocha mwenyewe basi ni viongozi.

Nilikuwa Nina miaka 12 wakati tunaondolewa na Caf kwenye michuano ya vijana kwa kumchezesha Nurdin Bakari mwaka 2005, kuanzia pale sikuona mpango wa vijana uliofanikiwa tena, unaweza kupata jibu?.

 Ninaikumbuka timu ya Copa Coca Cola iliyoenda kushinda Brazil,  lakini watafute wangapi waliingia katika mfumo wa taifa mpaka leo, Tumetega ngazi tukaenda kulala, tunataka kuamka tujikute pale juu yake katika kilele.  Nani alikuambia inawezekana?.tz

Hata Mungu hatoi bahati za namna hii, Hakuna anayeokota pesa chumbani kwake,  na hakuwepo aliyefanikiwa kuivisha chakula chini ya uvungu. Acha tuendelee kulala,  tusubiri kupanda ngazi ya kufikirika. Wakati tunastuka Tahiti atakuwa robo fainali kombe la dunia. Ahsanteni



Comments