STAND UNITED; ‘Tupo eneo la hatari, ila tutatimiza malengo yetu msimu huu…’



STAND UNITED; 'Tupo eneo la hatari, ila tutatimiza malengo yetu msimu huu…'

stand fNa Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,

Stand United iko katika nafasi ya 13 ( nafasi ya mwisho kwa timu zitakazoshuka daraja). Timu  hiyo ya Shinyanga inacheza ligi kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza msimu huu. Ni miongoni mwa timu tatu ' changa' zaidi katika ligi ya Bara. Ukitoa timu za Azam FC, Mbeya City na Ndanda FC, Stand ni timu iliyoanzishwa mwaka 2012 na kupanda ligi kuu msimu huu.

Ikiwa imecheza michezo 19  hadi sasa timu hiyo itacheza na Mtibwa Sugar, Polisi Morogoro na JKT Ruvu katika uwanja wa nyumbani ( Kambarage Stadium) kabla ya kuja Dar es Salaam kuwakabili ' wababe wa ligi' Yanga SC katika uwanja wa Taifa, kisha mabingwa watetezi Azam FC katika dimba la Chamanzi Complex. Baada ya michezo hiyo miwili ya Dar, Stand itasafiri hadi Tanga kuwakabili Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani kabla ya kurejea nyumbani siku ya mwisho ya msimu kuwakabili Ruvu Shooting.

" Ratiba inatutega. tunatakiwa tushinde mechi Tatu,  hizi za nyumbani dhidi ya Mtibwa, JKT Ruvu na Polisi Moro kabla ys kwenda kuwavaa Yanga, Azam, Coastal na kumaliza tena nyumbani na Shooting" anasema Muhibu Kanu, mkuu wa idara ya ufundi ya timu hiyo wakati alipofanya mahojiano na mwandishi wa mtandao huu.

" Hatuko katika nafasi nzuri sana,  ila lengo la msimu huu ni kubakisha timu kwenye ligi. Naamini tutalifikia lengo hilo kisha kuja na ' plan mpya msimu ujao'"

Ni tofauti ya alama nne tu kati ya Stand na timu iliyo nafasi ya nne Kagera Sugar, huku kukiwa na timu zilizocheza mchezo mmoja zaidi, Coastal,  Ndanda FC na Ruvu Shooting, vita ya kuhepuka kushuka msimu huu itakuwa ni kali kuliko misimu yote. Timu mbili za mwisho zitashuka daraja na wakati huu Tanzania Prisons wakiburuza mkia wakiwa na alama 17 baada ya kucheza michezo 1 ni wazi Stand inatakiwa kushinda michezo ya minne ya nyumbani iliyosalia.

" Ligi ina ushindani sana.na inatakiwa iwe hivi hivi ili  tuwe na ligi bora,  ila baadhi ya waamuzi wanataka kuiharibu. Ukiwa na ligi bora hata timu yako ya Taifa inakuwa bora. Ili tuwe na wawakilishi wazuri katika michuano ya kimataifa ni lazima tuwe na ligi kama hii, waamuzi tu baadhi wanatakiwa kusimamia vizuri"

Kama timu inayocheza ligi kuu kwa mara ya kwanza, mmejifunza kitu gani, kiufundi, kimbinu na hata nje ya uwanja kwa maana ya utawala?

" Shinyanga hatujawahi kuwa na timu ya ligi kuu kwa zaidi ya miaka 18 iliyopita. kiutawala viongozi wanajifunza jinsi ya kuishi na wachezaji, hiki ni kiwanda kipya kwao hivyo mambo mengi ni mageni.  Kiufundi tumejifunza mengi zaidi ni jinsi gani unaweza kuutafuta ushindi katika viwanja vya ugenini na nyumbani. Ugenini,  ili ufanikiwe wachezaji uwaweke katika hali gani ya maisha.kabla ili tufanikiwe, kufanya usajili kuendana na malengo ya mbele ya klabu." Anasema Muhibu ambaye anawasisitiza wapenzi wa soka Mkoani Shinyanga kuiunga mkono timu hiyo kwa kujitokeza uwanjani kila inapocheza katika uwanja wa Kambarage, Stand pia kwa upande wao wamekerwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya ratiba;

" Vitu ambavyo hatujavutiwa navyo msimu huu ni uamuzi na kubadilika kwa ratiba mara kwa mara. Lakini napenda kuwaambia wapenzi wa Stand waiunge mkono timu yao. waje kwa wingi uwanjani tarehe  5 wakati wa mchezo dhidi ya Mtibwa"



Comments