SIKILIZA ASHA BARAKA ALIVYOMPIGA DONGO NYOSHI NA FM ACADEMIA …amwambia muziki si mavazi, amtaka akumbuke alivyomleta Bongo akiwa hajui kuvaa
Mkurugenzi wa Aset inayomiliki Twanga Pepeta, mamaa Asha Baraka amemtupia dongo zito rais wa FM Academia Nyoshi el Sadaat.
Asha Baraka amemtaka Nyoshi na FM Academia yake watambue kuwa muziki si mavazi na wajiandae kupokea kichapo siku ya mpambano wao Jumamosi hii pale Escape One Mikocheni.
Mkurugenzi huyo amemtaka Nyoshi akumbuke alivyokuja Tanzania kwa mara ya kwanza na namna alivyokuwa hajui kuvaa.
"Nilimleta Nyoshi Tanzania akiwa hajui kuvaa, ninazo picha zake, kama kuvaa kajulia Bongo kwahiyo aache kabisa kuiambia Twanga Pepeta haijui kuvaa, muziki si mavazi," alisema Asha Baraka katika maongezi yake na Saluti5.
Msikilize zaidi Asha Baraka hapo chini.
Comments
Post a Comment