Hart akibasamu mbele ya Lionel Messi
PAUL Scholes amemkosoa Joe Hart kwa kitendo chake cha kufurahia licha ya Manchester City kutolewa na Barcelona katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.
Hart alikuwa kwenye kiwango cha juu Nou Camp siku ya jumatato wiki hii kwa kuokoa michomo mingi na kuifanya Barca asivuna magoli mengi.
Barcelona walishinda mechi ya pili, shukuruni kwa bao pekee la kipindi cha kwanza la Ivan Rakitic na Wakatalunya hao walisonga kwa tofauti ya magoli 3-1.
Hart aliokoa michomo mingi na kuzuia magoli mengi Nou Camp
Akiandika katika kolamu yake ya gazeti la Independent, Scholes alisema: "Kazi nzuri Joe Hart kwa kufanya kazi kubwa ya kuokoa michomo mikali msimu huu ligi ya mabingwa, na bila yeye mambo yangekuwa mabaya zaidi kwa City".
"Lakini kitu kimoja kisichoniingia kichwani ni ushahidi wa yeye kufurahia. Baada ya mechi kumalizika alifurahia kila alipookoa na kuwashangilia na mabeki wake.
"City walikuwa wanapoteza 1-0. Walikuwa wanatupwa nje ya ligi ya mabingwa. Walikuwa wanashangilia nini? kupoteza 5-0?
Comments
Post a Comment