Robben, Ribery Kuiponza Bayern kesho


Robben, Ribery Kuiponza Bayern kesho

robben800-1321010855Na Amplifaya Amplifaya

Klabu ya soka ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani imepata pigo mara baada ya wachezaji wake tegemeo mholanzi Arjen Robben na mfaransa Frank Ribery kupata majeruhi katika mchezo wa juzi dhidi ya Shakhtar Donetsk katika michuano ya klabu bingwa ulaya(UEFA) ambapo Bayern ilishinda magoli 7-0.

Robben ambaye mpaka sasa ndio mfungaji bora wa timu hiyo msimu huu ambapo tayari ameshafunga magoli 17 alishindwa kuendelea na mchezo huo mara baada ya kupata majeruhi katika dakika ya 19 hivyo kutolewa na kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi.

Mfaransa Ribery alishindwa kuendelea na mchezo huo katikati mwa kipindi cha pili baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu ambapo alifunga goli moja kati ya saba yaliyofungwa na timu hiyo.Franck-Ribery-150311-Substitute-G-300

Sasa wachezaji hao watakosa mchezo wa ligi kuu nchini Ujerumani siku ya jumapili dhidi ya Weder Bremen na huku wapinzani wao
walionafasi ya pili timu ya VfL Wolfsburg itakuwa ikipambana na Freiburg.

Mpaka sasa Bayern Munich inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 61 katika michezo 24 iliyocheza pointi 11 zaidi ya Wolfsburg iliyonafasi ya pili ikiwa na pointi 50 huku Borussia Mönchengladbach ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 41 na nafasi ya nne ikishikwa na Bayer
Leverkusen iliyo na pointi 39 huku timu zote zikiwa zimecheza michezo 24 kila mmoja.



Comments