Robben atakosekana uwanjani kwa muda wa wiki kadhaa



Robben atakosekana uwanjani kwa muda wa wiki kadhaa

26E5AF7E00000578-3006685-image-a-13_1427051152372Na Augustino Mabalwe,Dar es salaam

Kiungo wa klabu ya Bayern Munich Arjen Robben atakosekana uwanjani kwa muda wa wiki kadhaa baada ya kuumia hapo jana katika mechi iliyoisha kwa mabingwa hao wa bundesliga kupokea kichapo cha  2-0 kutoka kwa Borrusia Monchenglabach licha ya kucheza katika uwanjani nyumbani Allianz Arena.

Mholanzi huyo alipata maumivu hayo katika dakika ya 24 ya mchezo baada ya kuchezewa vibaya na beki Tony Jantske na hivyo kutolewa nje akiwa amebebwa kwenye machela.

Hii ni habari mbaya kwa Arjen Robben ambaye amerudi mazoezini hivi karibuni baada ya kuumia katika mechi ya klabu bingwa dhidi ya Shaktar Donetsk Machi 12.

Kocha wa klabu hiyo mhispania Pep Guardiola anakibarua kizito kuziba pengo la winga huyo machachari ambaye anauwezekano mkubwa wa kukosa mechi za robo fainali za klabu bingwa Ulaya dhidi ya FC Porto mwezi ujao.

Aidha Robben,31, atakosa mechi ya timu ya taifa ya uholanzi dhidi ya Uturuki ambayo ni mechi ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya mataifa Ulaya mwaka 2016 na ile ya kirafiki dhidi ya Hispania.

 


Comments