PSG imelipa Kisasi kwa Chelsea baada ya kuwatoa mwaka jana kwa mabao yale yale


PSG imelipa Kisasi kwa Chelsea baada ya kuwatoa mwaka jana kwa mabao yale yale

silva 2Na Amplifaya
Hakuna mchezaji yoyote wa Chelsea aliyemzidi David Luiz magoli msimu huu katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Rickie Lambert ana magoli mengi kuliko Diego Costa kwenye michuano ya klabu Bingwa Ulaya msimu huu.

Mwaka jana Chelsea iliitoa PSG kwa sheria ya bao la ugenini baada ya kufungana 3-3 mechi mbili. Mwaka huu PSG imeitoa Chelsea kwa staili hiyo hiyo huku matokeo yakiwa yale yale 3-3 kwa mechi mbili.

David Luiz aliiwezesha Chelsea kuitoa PSG mwaka 2014. Mwaka huu ameiwezesha PSG kuitoa Chelsea.

Chelsea ndio timu iliyopewa penati nyingi zaidi msimu huu katika michuano ya UEFA Champion League kuliko timu zote (5).



Comments