Klabu ya Tanzania Prisons kutoka Jijini Mbeya, Leo imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono dhidi ya Stand United baada ya kuichapa kwa jumla ya mabao 3-0 katika Uwanja wa Sokoine ikiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Prisons ambao wanashika mkia wa VPL, wamejikuta wakiiadhibu timu hiyo kutoka Shinyanga kwa jumla ya mabao matatu mtungi (3-0).
Hata hivyo licha ya kupata ushindi huo, Wajelala hao bado hawajafanikiwa kujinasua katika mkia wa ligi kwani leo wamefikisha pointi 16.
Katika viwanja vingine, Coastal Unio imegawana pointi moja na Ruvu Shooting baada ya kutoa sare ya bao 1-1 katika Uwanja wa Mabatini Mlandizi, Mkoani Pwani.
Kwa upande wa Polisi Morogoro ambao walikuwa wenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Jamhuri, walijikuta wkiambulia kipigocha bao 1-0.
Comments
Post a Comment