PICHA 20: ACHANA KABISA NA MZEE YUSSUF ...ashusha mjengo wa maana, mradi wake wa matofali nao usiseme
Mzee Yussuf anaweza kuwa mfano mzuri sana kwa wanamuziki wengine kwa namna anavyowekeza ili asitetereke pale atakapoamua kuupa mkono wa kwaheri muziki au muziki kumpa mkono wa kwaheri.
Mfalme huyo wa taarab anayemiliki kundi la Jahazi Modern Taarab, ana mradi mkubwa wa kuuza vifaa vya ujenzi ikiwemo cement na mtofali ya kisasa huko Chanika na Kigamboni.
Mzee Yussuf ana viwanja viwili vyenye mradi wa kufyatua matofali huko Chanika na kimoja kingine Kigamboni. Ni miradi mikubwa ambayo iko chini ya mwamvuli wa kampuni yake inayojulikana kama M.Y. Contractors.
Katika kurahisisha kazi za M.Y. Contractors, Mzee Yussuf anamikili malori ya Scania na Fuso ambayo hutumika kubeba michanga, matofali na vifaa vingine kwaajili ya viwanda vyake pamoja na wateja wake.
Hakika Mzee Yussuf yuko vizuri sana kwani Saluti5 ilipotembelea moja ya viwanja vyake vya Chanika, ikashuhudia ujenzi wa mjengo wa maana utakaokuwa na gorofa moja kwaajili ya makazi yake na familia yake.
Lakini ndani ya uwanja huo mkubwa unaoweza kujenga hata nyumba 20 za kawaida, kuna nyumba nyingine ya maana ambayo nayo ujenzi wake haujakamilika. Ni nyumba mbili za maana kwa mpigo, achalia mbali jengo lenye maduka na ofisi yake.
Katika kuonyesha kuwa kiwanja hicho ni kikubwa kupindukia, sehemu ya mbele Mzee Yussuf amejenga jengo lenye maduka manne ambayo yote yatahusiana na kazi za M.Y. Contractors lakini pia nyuma ya maduka hayo kuna vyumba vingine ambavyo vitatumika kama ofisi yake na maafisa wengine wa kampuni.
Mzee Yussuf ameidokeza Saluti5 kuwa ameanzisha pia mradi mkubwa wa kufuga kuku wa nyama na mayai (wa kisasa na kienyeji) huko Kigamboni.
Kwa namna alivyowekeza Mzee Yussuf, hakuna ubishi kuwa nyota huyo sasa anaweza kabisa kuishi bila kutegemea pato la muziki.
Hii ni nyumba nyingine ya Mzee Yussuf ambayo ipo kwenye uwanja wake huo huo wa Chanika
Comments
Post a Comment