PICHA 14 ZA ISHA MASHAUZI ALIVYO BEEP UJIO WA USIKU WA BABA NA MWANA JUMAPILI ILIYOPITA KWENYE SHOW YA JAHAZI …mzigo kamili ni Jumapili hii Travertine Magomeni
Jumapili iliyopita baada ya show ya Usiku wa Baba na Mwana kuahirishwa kutokana na tishio la mvua, Jahazi Modern Taarab wakafanya onyesho lao la kawaida la kila Jumapili ndani ya Travertine Hotel Magomeni.
Lakini Isha Mashauzi akaibuka ukumbini hapo na kuwaonjesha mashabiki kile watakachokipata katika Usiku wa Baba na Mwana ambao sasa utafanyika Jumapili hii tarehe 29 hapo hapo Travertine Hotel.
Isha akaimba "Yawenzenu Midomoni" moja ya nyimbo zilizompa jina katika Jahazi. Ukumbi ukalipuka kwa mayowe.
Mwimbaji huyo akawaimbisha mashabiki vile alivyotaka, wakatikia kila alichowaimbisha.
Hata pale alipogusia vipande vvya nyimbo zake ukiwemo "Sura Surambi" bado mashabiki wakageuka kuwa waitikiaji.
Onyesho la Baba na Mwana ambalo litazikutanisha bendi za Jahazi na Mashauzi Classic linafanyika Jumapili hii ambapo litafungwa jukwaa kubwa ili kumwezesha kila mshabiki kushuhudia burudani hiyo bila bughudha.
Kisayansi, hakuna tishio la mvua kwani utabiri wa hali ya hewa kwa siku tano zijazo unaonyesha kuwa Jumapili asubuhi kutakuwa na mvua kidogo na pamoja na wingu zito kiasi na jioni saa 12 kutakuwa na manyunyu ya hapa na pale ambayo yatakata baada ya muda mfupi na baada ya hapo hakutakuwa tena na mvua wala manyunyu hadi kunapambazuka.
Pata picha 14 za Isha Mashauzi alivyofanya makamuzi kwenye jukwaa la bendi yake ya zamani.
Comments
Post a Comment