PEPE REINA AMTAKA DE GEA ABAKIE MANCHESTER UNITED NA KUITOSA REAL MADRID



PEPE REINA AMTAKA DE GEA ABAKIE MANCHESTER UNITED NA KUITOSA REAL MADRID

David De Gea has been linked with a move to Real Madrid              as a replacement for Spain team-mate Iker Casillas

Kipa wa Bayern Munich Pepe Reina amesema David de Gea ni mmoja wa makipa bora barani Ulaya na hapo hapo kumtaka mlinda mlango huyo kubakia Manchester United licha kuwaniwa na Real Madrid.

De Gea ambaye alijiunga na United mwaka 2012 akitokea Atletico Madrid, alisota kuzoea maisha ya Premier League lakini sasa ni moja ya 'silaha' muhimu za Louis van Gaal msimu huu.

De Gea has been one of Louis van Gaal's most consistent              performers at Manchester United this seasonĀ 

Kiwango chake kwa misimu miwili iyopita kilikuwa bora huku akiokoa michomo ya hatari katika namna ya kushangaza na sasa Real Madrid inaamini De Gea ndiye mtu sahihi wa kumrithi kipa Iker Casillas.

Lakini Reina, nyota wa zamani wa Liverpool amesema De Gea anatakiwa aachane kabisa na mpango wa Real Madrid.

Pepe Reina has urged de Gea to stay put at Manchester              United despite interest from the La Liga giants

"Ni mmoja wa makipa bora Ulaya na 'fomu' yake msimu huu ni ya hali ya juu, Reina aliiambia talkSPORT.

"Pengine Real Madrid inasaka kipa mpya na De Gea ni moja ya majina yanayotajwa, lakini nadhani atakuwa na furaha zaidi kwa kuichezea Man United."



Comments