Pele: Neymar ni mwanangu, Sina Shaka na Messi


Pele: Neymar ni mwanangu, Sina Shaka na Messi

pele messNa Amplifaya Amplifaya

Unapata maana ya kwamba Pele anatambua kile au ni kipi unataka kumuuliza hata kabla haujaanza kubuni maneno.

Labda ni kitu asili chenye muingiliano na uelewa sawa wenye athari kwa tabia za binadamu na jinsi gani anaweza kutumia hiyo fursa kwa faida yake ambayo imemfanya kuweza mchezaji mkubwa na mwenye historia kubwa duniani pia mwenye rekodi ya kuwa mfungaji mwenye magoli mengi duniani ambapo katika mchezo wa soka haijawahi kutokea.

Au labda kiurahisi ni kama sababu ya marejeo au kitu kisichoweza kuepukika kimazoezi.

Mchezaji huyo ambaye ni mshindi mara tatu wa kombe la dunia akiwa na timu yake ya Taifa ya Brazil labda hakumbuki amefanya mahojiano mara ngapi na vyombo vya habari na jinsi alivyotambulika katika umma wa watu duniani, magoli yake ambayo yanahesabika kuwa ni 1284 katika michezo yake yote aliyocheza na ikiwa kama amepata stashahada ya rekodi ya dunia.

Pele atakuwa anafikisha miaka 75 mwaka huu (amezeeka sasa) lakini haoneshi dalili yotote ya kupumzika na kuachana na masuala ya soka maana amekuwa akijumuishwa katika masuala mengi ikiwemo matangazo, projekiti nyingi kuhusiana na soka kiujumla huku akizunguka takribani dunia nzima.

Hauhitaji kujitambulisha mwenyewe na kila mtu anajua Pele ni nani.

Mwishoni mwa wiki iliyopita moja kati ya majukumu yaliyompeleka Pele Uingereza alikuwa ni mmoja kati ya wageni maalum pale Anfield ambapo Liverpool iliwakaribisha Manchester United na mchezo kumalizika kwa Liverpool kufungwa mechi hiyo katika ligi kuu ya Uingereza.

"Ni furaha kuwa hapa" Pele alisema wakati akiongea na mwandishi mmoja wa habari"

"Kuja Uingereza zaidi ya mara moja ni kitu cha kujivunia zaidi" Pele alisema.

Brazil huwa tuna kila mechi kila ifikapo mwisho mwa wiki kupitia video na Uingereza pia ambayo ni ligi moja muhimu sana hapa Duniani. AlisemaNeymar

Kunaweza kuwa na baadhi ya wachezaji wengi wa Kibrazil ambao wanatumikia maisha yao ya soka na vilabu ya Uingereza lakini nyota wakubwa watabakia kuwa nyota wa kipekee, na hapo ndipo mazungumzo yalipogeukia kwa Neymar ambaye ndiyo anaaminiwa na Pele kuwa ni nyota wa Barcelona hasa kwa hizi siku zijazo za usoni akiwa na maana ya miaka ijayo mbele.

"Hakuna jipya, nineongea sana kuhusu Neymar" Pele alisema

"Ni kama mtoto wetu tu, alichezea Santos, nilichezea Santos na mwanangu Edinho alichezea Santos kama golikipa na hivyo tunafurahia kuwa na Neymar

Nadhani kiwango chake tokea mwaka jana hadi sasa kimeimarika zaidi na bado ana mambo mengi zaidi ya kujifunza akiwa kama mchezaji japo ni mchezaji mzuri"  Pele alisema.

Kumbuka kuwa Pele alishawahi kuwa mmoja wa watu waliopinga sana Neymar asiondoke Barcelona ili kulinda kiwango chake ndani ya Kilabu cha Santos na sio Barcelona tu halikadhalika Real Madrid na vilabu vingine.

Itakuwa ni kitu cha kujivunia zaidi kucheza Barcelona sababu Barcelona sio timu tu bali ni Messi na Neymar, Pele alisema kuwa Messi ni mchezaji bora ambaye hajawahi kumuona katika maisha yake ya soka na anasema licha ya kuwa Barcelona bado kuna wachezaji wengine ambao ni nguzo ya timu kama Xavi na Iniesta jinsi wanavyocheza wana mchango mkubwa sana katika timu.

Pele pia alizungumzia suala la FIFA kubadili ratiba ya kombe la dunia kwa mwaka 2022 ambapo litakuwa linachezwa majira ya masika mwezi wa 12.

" nadhani wiki hii ndiyo wameamua kombe lichezwe mwezi wa 12 kipindi ambacho kitakuwa ni cha majira ya joto kwetu Brazil, kitu kizuri ni kuliweka kombe katika mazingira mazuri kwa watu, mahali na wakati sio jambo muhimu bali ni kitu ambacho kinachanganya mno, mabadilikobya kucheza mwezibwa 12 sio madogo kabisa" Pele alisema.



Comments