Kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Scholes amesisitiza kuwa kocha wa Arsenal Arsene Wenger alikuwa sahihi kusema kuwa yeye (Scholes) angependa kucheza na kumsajili Mesut Ozil.
Wiki iliyopita Wenger alimkoromea Scholes kwa kauli yake ya kukosoa nyendo za Ozil, lakini sasa gwiji huyo wa Manchester United ana lingine la kusema baada ya Arsenal kuitoa United kwenye michuano ya FA Cup.
Scholes ameandika katika gazeti la The Independent: "Nimejikuta nikikubaliana na maneno ya Wenger.
"Wenger alisema Ijumaa iliyopita kuwa mie ningependa kucheza kando ya Ozil – na hiyo ingekuwa sahihi ili mradi tu kama Ozil angecheza soka bora kama alilocheza dhidi ya United Jumatatu usiku.
Comments
Post a Comment