NINI KINAMSIBU FABREGAS? KILA NUSU YA PILI YA MSIMU LAZIMA APOROMOKE KIWANGO


NINI KINAMSIBU FABREGAS? KILA NUSU YA PILI YA MSIMU LAZIMA APOROMOKE KIWANGO

The talented playmaker had a blistering start to the              season and has racked up 15 assists despite his slump

Pengine bado haijajulikana ni nini huwa kinamkumba kiungo Cesc Fabregas lakini ukweli ni kwamba kila nusu ya pili ya msimu huwa si yule wa nusu ya kwanza …hufifia kama mshumaa.

Fabregas aliyeingia Chelsea kwa kishindo akifunga na kusaidia kutengeneza magoli kibao huku akitesa na pasi zenye macho, amefunga bao moja na kusaidia mawili tu katika nusu ya msimu ukilinganisha msaada wake wa magoli 15 mwanzoni mwa msimu.

Fabregas hajahusika katika goli lolote ndani ya mechi tisa mfululizo za mwisho.

Lakini hata hivyo nyota huyo wa Chelsea aliyesajiliwa kutoka Barcelona, bado anaongoza kwa kusaidia kuzalisha magoli, yuko mbele mara saba kwa anayemfuatia, hii ni kutokana na hazina nzuri aliyojitengenezea katika nusu ya kwanza ya msimu.

Swali kubwa hivi sasa ni je Fabregas ataimarika na kumaliza msimu vizuri au ndiyo itakuwa yale yale kama ilivyokuwa kwenye enzi zake za Barcelona na Arsenal.



Comments