Ngassa: ‘Nikiifunga Kagera Sishangilii’


Ngassa: 'Nikiifunga Kagera Sishangilii'

NGASSA KILIO1Na. Richard Bakana, Dar es Salaam

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga pamoja na Timu ya Taifa ya Soka Tanzania , Mrisho Ngassa amesema kuwa endapo ataifunga Kagera Sugar leo hataweza kushangilia.

Akizungumza na Shaffihdauda.com Ngassa amesema kuwa Kagera Sugar ni timu yake ya kwanza katika maisha yake ya Soka ambayo alipelekwa na marehe Sylvester Marsh ambaye anazikwa leo huko Jijini Mwanza, hivyo ikitokea akafunga goli hataweza kushangilia kutokana na kuwa katika majonzi ya kupotea mtu muhimu katika maisha yake.

Ngassa amesema kuwa Kocha huyo ndio aliyemfungulia Maisha ya soka akiwa bado Mtoto hivyo hataweza kushangilia atakapokutana na timu ambayo pia amewahi kuifundisha kocha huyo kwani atakuwa bado  anamajonzi.

"Kifo cha Marsh naamini ni pigo kwa Tanzania, leo tunakutana na Kagera Sugar naamini itakuwa ni mechi nzuri kwasababu Marsh alinipeleka Kagera, Sitaweza kushangilia kwasababu bado tupo katika majonzi" Amesema Ngassa ambaye alikuwa kambini akijiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Kagera Sugar katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza namna alivyokutana na Marsh, Ngasa amesema hivi "Marsh ndiye aliyenileta timu ya Taifa yavijana ya U17 , na baada ya U17 akanipeleka Kagera Sugar na baadaye akafanya mipango nikaenda Yanga ambapo pia alinileta timu ya Taifa ya Wakubwa, Hadi hapa nilipofikia yeye anamchango mkubwa sana, hata kipindi naenda Yeye ndio alikuwa ananifundisha mazoezi binafsi hadi nikawa Mfungaji bora, kwahiyo ni Mtu ambaye alikuwa karibu yangu toka nipo mdogo".ngassa na MarshNgassa kafunguka namna ambavyo walikutana na Marsh hadi kufikia kufanya kazi pamoja.

"Ilikuwa ni katika mashindano ya watoto chini ya miaka 15-8 ambapo mimi nilikuwa nachezea timu ya Beach Boys pamoja na Mwinyi, Jerry alikuwa timu ya Jonas na Henry Joseph alikuwa timu ya Channel, kwahiyo Marsh alikuwa ndio Mtu anayechukua Vipaji na kuwapeleka Sehemu Nyingine kuviendeleza na ndipo Marsh alinichukua katika Academy yake akaanza kunifundisha ndio kunipeleka Serengeti Boys" Amesema Ngassa ambaye leo ataongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga dhidi ya Timu yake ya Kwanza katika ligi kuu ya Bongo Kagera Sugar.

Kwa upande wake Nyota wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania ambaye kwa sasa kama amesahaulika Jerry Tegete, ambaye ni rafiki mkubwa wa Ngassa toka wadogo, amesema kuwa Marsh ndio aliyemmulika hadi kuonekana na kuchukuliwa katika kikosi cha timu ya Taifa chini ya Marcio Maximo.TEGETE (1)"Mimi nakumbuka wakati nipo Makongo, Walichagua timu ya Vijana yeye akiwa Kocha, akampigia Simu Marehemu Matokeo, akaniambia niende mazoezini Karume aniangalie nikifanya vizuri nitachukuliwa timu ya Taifa ya Vijana, kulikuwa na mechi Burundi, Nilienda mazoezini nikakubarika ndio nikaondoka na timu hadi Burundi nikiwa mshambuliaji,

"Hapo ndio mafanikio yakaanza, Wakati nafanya mazoezi Karume Maximo ndio aliniona kwahiyo akasema akirudi huyu itabidi abaki azidi kufanya mazoezi na wakubwa, kwahiyo hapo ndio nikawa nimeonekana ndio ikawa moja kwa moja" Amesema Jerry Tegete ambaye pia amepitia kwenye mikono ya Marsh ambaye anazikwa leo Jijini Mwanza.



Comments