Baada ya kukalia usukani wa upachikaji wa mabao katika ligi ya Vodacom Tanzania bara mshambuliaji wa Azam Fc Didier Kavumbagu leo amekubali kushushwa katika kiti hicho na Simoni Msuva wa Yanga.
Msuva amemshusha Kavumbagu ambaye ana magoli 10 baada ya leo kuifungia Yanga mabao mawili(2) kati ya matatu(3) kwenye ushindi wa bao 3-1 dhidi ya JKT Ruvu na kufikisha jumla ya magoli 11 juu zaidi katika mbio za kusaka kiatu cha mfungaji bora wa ligi.
Huu ndiyo msimamo wa wafumania nyavu katika ligi kuu.
Comments
Post a Comment