Msuva aibeba Yanga Taifa, waichapa JKT Ruvu 3-1



Msuva aibeba Yanga Taifa, waichapa JKT Ruvu 3-1

Msuva..Mshambuliaji wa kilabu Yanga Simoni Msuva leo ameibuka kinara wa mchezo baada ya kuifungia timu yake mabao mawili kati ya matatu (3-1) dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo ambao JKT Ruvu walikuwa wenyeji walijikuta wakiambulia kipigo kunako dakika 34 kwa mkwaju wa penati uliotupiwa kambani na Msuva.

Kunako dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza mshambuliaji wa zamani wa Polisi Morogoro Danny Mrwanda akimalizia kazi nzuri kutoka kwa Msuva ambaye alipokea pasi ya Ngassa, aliiandikia Yanga bao la pili ambapo haikuchukua muda mrefu JKT Ruvu wakajipatia bao kupitia kwa Kamuntu zikiwa zimebakia dakika 2 mchezo huo kumalizika ndani ya dakika 3 za nyongeza na kufanya timu hizo kwenda mapumziko Yanga ikiongoza 2-1.

Ikiwa ni katika harakati za kuendelea kujiweka kilele mwa ligi hiyo ya Tanzabia Bara, Simoni Msuva kwa mara ya pili akaiandikia Yanga bao la 3 kufuatia uzembe wa mabeki wa JKT Ruvu kunako dakika ya 57 kipindi cha pili na cha lala salama.

Mshambuliaji wa JKT Ruvu Kamuntu licha ya kuipatia timu yake bao la kufutia machozi, alijikuta akizawadiwa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa kilabu ya Yanga pamoja na Taifa Stars Mrisho Khalfan Ngassa.



Comments