MSIKILIZE NYOSHI ALIVYOJIBU MAPIGO KWA ASHA BARAKA …akiri alikuja Bongo na nguo moja tu ya kubadilisha lakini aitaka Twanga ijiandae na kipigo, awashangaa kuweka kambi

Rais wa FM Academia Nyoshi el Sadaat (pichani kushoto) amemtaka Asha Baraka aache kutapa tapa na badale yake asubiri aibu kutoka kwa FM Academia Jumamosi hii ndani ya Escape One.

Akiongea katika ofisi za Saluti5, Nyoshi akasema kamwe hajawahi kutambia mavazi katika kuelekea mpambano wao, bali siku zote amekuwa akiamini kuwa silaha kubwa ya FM Academia ni muziki ulioenea kila idara kuanzia show, uimbaji hadi kwenye vyombo.

Rais huyo amesema Twanga ni bendi kubwa lakini hawana haja ya kuiwekea kambi kwa wanajua ni sehemu gani ya kuwamaliza.

Nyoshi pia amekiri ni kweli kuwa alikuja bongo na nguo moja tu ya kubadilisha lakini ni kutokana na kutoroka nyumbani kwao ili kuja kusaka maisha Tanzania.

"Wazazi wangu walikuwa wanamiliki duka kubwa la nguo kutoka Paris na sehemu nyingine kwa hiyo nguo halikuwa tatizo kwangu, ila hawakutaka niwe mwanamuziki hivyo nikatoroka bila kubeba begi la nguo," anafafanua Nyoshi.

Hakika huwezi kuyafaidi maneno ya Nyoshi kwa maandishi haya, hebu msikilize mwenyewe hapo chini upate mengi zaidi pamoja na kuvunja mbavu zako.

Comments