Mesut Ozil amesema ana furaha Arsenal na ametupilia mbali tetesi za uwezekano wa kutimka kwa washika bunduki hao wa London.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia ambaye alijiunga na Arsenal mwaka 2013 kwa ada ya pauni milioni milioni 42 iliyovunja rekodi ya klabu na ambaye aling'ara katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wiki hii dhidi ya Monaco, amesema lengo lake ni kuiletea mafanikio klabu yake.
Ozil amelieleza gazeti la Express la Ujerumani: "Kurejea Ujerumani si lengo langu kwa sasa. Nina furaha sana Arsenal na nataka kuendelea kuwa hapa.
"Nimecheza Bundesliga, nimeichezea pia Real Madrid katika La Liga. Lakini Ligi Kuu ya England ni ligi ngumu zaidi duniani. Kamwe wapinzani wako hawakati tamaa."
Comments
Post a Comment