Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakikunjana baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na www.superdboxingcoach.
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Mada Maugo na Kalama Nyilawila nusula wazipige kavu kavu wakati wa upimaji wa uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kesho jumapili mpambano utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa wakati wa upimaji uzito.
Maugo alienda kumtambia Kalama na kumpiga kibao pamoja na teke kali sana lililompiga Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakati akiamulizia ugomvi huo, ndipo lilipozuka songombingo kali kwa mashabiki wa kambi zote mbili wakitaka kuzipiga kavu kavu huku Maugo akiwa ameshapanda moli wa kupigana nje ya uringo.Bondia Thomas Mashali akipima uzito.
Mpambano huo ambao utakuwa na michezo mingine ya kumaliza ubishi ni kati ya Thomas Mashali atakayemkabili Abdallah Pazi na Japhert Kaseba atapambana na Saidi Mbelwa mapambano hayo yote yatafanyika siku ya jumapili march 15 (Kesho) katika uwanja wa ndani wa taifa ambapo baadhi ya mashabiki wameomba baadhi ya daladala zinazofanya kazi usiku kwenda kuwa chukuwa pindi wamalizapo kuangalia mapambano hayo yaliyo na ushindani wa kweli.
Comments
Post a Comment