MASHAUZI CLASSIC KURINDIMA MWANZA LEO USIKU …Isha Mashauzi kunadi ngoma zake za rhumba

MASHAUZI CLASSIC KURINDIMA MWANZA LEO USIKU …Isha Mashauzi kunadi ngoma zake za rhumba
MASHAUZI CLASSIC KURINDIMA MWANZA LEO USIKU …Isha            Mashauzi kunadi ngoma zake za rhumba

Wakali wa miondoko ya modern taarab, Mashauzi Classic leo usiku watakuwa Mwanza mjini katika onyesho kubwa litakalofanyika ndani Buzuruga Plaza.

Katika moja ya mambo yanayotarajiwa kutingisha onyesho hilo, ni pamoja na utambulisho wa nyimbo mbili za Isha Mashauzi zilizoko katika miondoko ya rhumba "Nimlaumu Nani" na "Nimpe Nani" ambazo zinafanya vizuri sana kwenye vituo vya radio.

Mashauzi Classic wamepaa leo asubuhi kuelekea Mwanza kwa ndege ya Fast Jet na wanatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam Jumapili mchana wa usafiri huo huo tayari kwa onyesho lao la pamoja na Jahazi Modern Taarab litalofanyika usiku huo kwenye ukumbi wa Travertine Hotel Magomeni.   

Comments