Marquinhos aoengeza mkataba PSG


Marquinhos aoengeza mkataba PSG

Marquinhos-v-Barcelona_3255658Na Augustino Mabalwe,Dar es salaam

Beki wa klabu ya Psg, Marco Marquinhos amesaini mkataba wa mwaka mmoja katika klabu yake,hivyo ataendelea kubakia kwa matajiri hao mpaka mwaka 2019.

Mbrazili huyo aliyehusishwa kujiunga na Manchester United mapema mwezi januari mwaka huu,kwa sasa mekuwa na kiwango kizuri tangu asajiliwe na klabu hiyo mwaka 2013 akitokea AS Roma. "Ninafuraha kwa hii hatua nyingine na inanipa nguvu ya kujiamini na kujituma zaidi. Psg imebadili maisha yangu na ninatumaini kuendelea kuwepo hapa kwa muda mrefu " alisema Marquinhos

Marquinhos mwenye umri wa miaka 20 aliisadia klabu hiyo kuchukua kombe la ligi kuu nchini Ufaransa msimu uliopita na mpaka sasa msimu huu ameshacheza timu hiyo mechi 31 na huku akionekana kuelewana na Mbrazili mwenzake Thiago Silva



Comments