MANGO GARDEN KUENDELEA KUIKOSA MALAIKA BAND KWA WIKI YA SITA …Ijumaa hii wako TCC Club, Ijumaa Kuu watakuwa mikoani

Bendi ya Malaika chini ya Mfalme wa masauti – Christian Bella, ambayo kwa kawaida hupiga Mango Garden kila Ijumaa, wiki hii watakuwa TCC Club Chang'ombe.

Hiyo itamaanisha kuwa Mango Garden watakuwa wanaikosa bendi hiyo kwa Ijumaa ya sita mfululizo.

Malaika walikuwa kwenye ziara ndefu ya mikoani iliyowafanya wakosekane Mango kwa takriban mwezi mzima, lakini mara waliporejea jijini, kinyume na ilivyotarajiwa na wengi kuwa Ijumaa ya tarehe 20 mwezi ingewakuta Mango Garden, lakini bendi hiyo ikawa na onyesho maalum Mzalengo Pub Kijitonyama.

Ijumaa hii ya tarehe 27, Malaika watakuwa TCC Club na Ijumaa ijayo watakuwa tena mikoani kwenye maonyesho maalum ya sherehe za Pasaka.

Comments