Manchester City imekuwa timu ya mwisho kutoka England kuaga michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kufungwa 1-0 na Barcelona kwenye mechi iliyochezwa Camp Nou.
Kwa kipigo hicho, City inakuwa imetolewa kwa jumla ya bao 3-1, hii ikiwa ni baada ya kukubali kipigo cha 2-1 nyumbani katika mchezo wa kwanza uliopigwa Etihad Stadium.
Bao pekee la Barcleona lilifungwa na Ivan Rakitic dakika ya 31 huku City ikipoteza nafasi ya kusawazisha dakika ya 78 pale mshambuliaji wake Sergio Aguero alipokosa penalti.
Timu zingine za England ambazo kama ilivyo City, nazo zikakomea hatua ya 16 bora ni Chelsea iliyong'olewa na PSG na Arsenal iliyofungishwa virago na Monaco.
Comments
Post a Comment