Kocha wa Mashetani Wekundu, Louis van Gaal amesisitiza kuwa Manchester United ni klabu kubwa duniani.
Mdachi huyo ambaye amewahi kuzikochi Barcelona na Bayern Munich, anasema hajawahi kukisia ukubwa wa United hadi pale alipojiunga nayo.
Akiongea na The Daily Telegraph, Van Gaal akasema: "United ni kubwa kuliko Real Madrid? Ndiyo. Kwa misingi ya kukubalika duniani, japo sio kihistoria."
Real Madrid ilitwaa taji lake la 10 la Ligi ya Mabingwa msimu uliopita wakati United ikiwa imefanya hivyo mara tatu tu.
Van Gaal akaendelea: "Nilizunguka na mke wangu sehemu kadhaa duniani ikiwemo China na Hong Kong na kushuhudia 'wazimu' wa ushabiki wa soka kwa katika nchi hizo.
"Wakanigundua kila nilipokwenda. Lilikuwa ni jambo la ajabu sana. Wanaijua Manchester United kuliko wanavyomjua kocha."
Comments
Post a Comment