Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Kocha mkuu wa AFC Leopards, Zdravko Logarusic ameshtushwa kuona wachezaji wake wanaingia uwanjani bila vizuia ugoko 'shin guards' katika mechi yao ya kirafiki ya jana Jumatano dhidi ya Moyas iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Katika mechi hiyo, Loga, kocha wa zamani wa Simba SC, alifanya mabadiliko mara 15 na katika kila badiliko, mchezaji aliyeingia uwanjani alilazimika kuchukua shin guards za mchezaji aliyetoka.
Baada ya kuulizwa na waandishi kuhusu hali hiyo, Mcroatia huyo alicheka na kusema kuwa wachezaji hawajitumi na hawastahili kuwa katika klabu kubwa kama hiyo.
"Nilishtuka baada ya kuwaona baadhi yao hawana shin guards. Kufanya hivyo, ni sawa na kuripoti kazini bila vitendea kazi, kwangu ni burudani ya aina yake,' amesema Loga.
Wachezaji wa timu hiyo pia hawakuwa na jezi zinazofanana kwa ajili ya mazoezi, jambo ambalo linaashiria kukosekana kwa weledi.
Comments
Post a Comment