Lionel Messi ndiye mwanasoka anayelipwa zaidi duniani, akiwa anaingiza karibu pauni milioni 1 kwa wiki kupitia mshahara pamoja dili za wadhamini.
Nyota huyo wa Argentina na Barcelona ameweka kibindoni pauni milioni 47.8 kwa mwaka 2014 ndani yake ikiwa ni mshahara wa pauni milioni 26 ukijaziwa na malipo ya kutoka kwa wadhamini adidas, FIFA 15 na Turkish Airlines.
Hiyo inamweka Messi mbali kabisa na mpinzani wake mkubwa Cristiano Ronaldo ambaye anashika nafasi ya pili kwa kuingiza pauni milioni 39.7 mwaka 2014, hii ikiwa ni kwa mujibu wa toleo jibya la jarida France Football.
Nyota mwingine wa Barcelona, Neymar amekaa nafasi ya tatu kwa kutia mkononi pauni milioni 26.8 akifuatiwa na Thiago Silva (£20.2m) huku Robin van Persie ambaye anakuwa ndiye mchezaji tajiri zaidi katika Premier League, akiwa kwenye nafasi ya tano kwa kuingiza pauni milioni 18.8.
Gareth Bale wa Real Madrid anafuatia kwa pauni milioni 17.5 na nyuma yake yupo nahodha wa Manchester United Wayne Rooney mwenye pauni milioni 16.5.
Wanaokamilisha Top Ten ni Zlatan Ibrahimovic, Sergio Aguero na Robert Lewandowski lakini wakiwa wanafuatiwa kwa karibu na Eden Hazard na Yaya Toure (wote-kila mmoja £14.7m), Angel di Maria na Radamel Falcao ambao kila mmoja amejikusanyia £13.6m.
1. Lionel Messi £47.8m
2. Cristiano Ronaldo £39.7m
3. Neymar £26.8m
4. Thiago Silva £20.2m
5. Robin van Persie £18.8m
6. Gareth Bale £17.5m
7. Wayne Rooney £16.5m
8. Zlatan Ibrahimovic £15.8m
9. Sergio Aguero £15.6m
10. Robert Lewandowski £14.8m
Comments
Post a Comment