Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
.SAIMON MSUVA……. Uandishi si Chungwa, ili waandishi waweze ' kuwakatia' wasomaji wote wapate kunja. Nadharia chache nitakazozitumia katika makala haya ya ' Jicho Langu la Tatu' kumuhusu kiungo-mshambulizi SAIMON MSUVA wa klabu ya Yanga SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars naamini zitatosha kuchochea mawazo yangu kwa msomaji wa makala haya.
Mvusa alifunga mabao mawili katika ushindi wa Yanga 3-1 JKT Ruvu siku ya jana Jumatano na kufikisha jumla ya mabao 11 katika ligi kuu Bara msimu huu. Pamoja na kufunga kwake, lakini Msuva alikuwa pia akiindesha timu na kuifanya Yanga kuongeza gepu la pointi kati yake na mabingwa watetezi Azam FC. Ushindi huo umewafanya Yanga kuwa mbele ya Azam kwa alama nne zaidi baada ya kucheza michezo 19 mchezo mmoja zaidi ya Azam FC).
Mtu mwingine anaweza kusema kuwa ushindi huo umekuwa muhimu zaidi kwa timu na si Msuva pekee, lakini wale wanaoangalia mbali zaidi wanamsifia Msuva kwa mchango wake mkubwa katika timu. Licha ya kutokea benchi na kutengeneza mabao mawili na kufunga moja wakati Yanga ilipoishinda Azam FC kwa mabao 3-0 katika mchezo wa Ngao Ya Jamii, Msuva alikosa nafasi katika kikosi cha kwanza mbele ya Andrey Coutinho na Mrisho Ngassa, lakini nyota huyo mwenye miaka 21 sasa aliendelea kutengeneza mabao na kufunga kila alipopewa nafasi na Marcio Maximo.
Anaweza kuwa katika nafasi ambayo shabiki au mtu yeyote anataraji atoe pasi kwa mchezaji aliye katika nafasi ya wazi zaidi, lakini hafanyi hivyo licha ya kwamba yeye ni kiungo, anajivika sifa za ushambuaji –uchoyo- na kujaribu kufunga Msuva amefunga mabao saba katika michezo mitano ya mwisho ya ligi kuu, mabao ambayo alifunga msimu wote uliopita 2013/14).
Kubwa zaidi ni kwamba mafanikio ya Msuva msimu huu ni ya kipekee nay a kujivunia pia kutokana na kucheza kama-' mfungaji na pia mpishi wa mabao'. Hilo linaweza kuwashangaza baadhi ya watu, lakini ukweli ni kwamba kiungo huyo ameamua kujipa jukumu la ufungaji, jukumu ambal katika hali ya kawaida linatakiwa kufanywa na mshambuliaji.
Siri ya kufanikiwa jukumu la ufungaji ni ' tabia yake ya kuwa mchoyo katika nafasi anazoweza kufanya uamuzi sahihi',. Mrisho Ngassa amekuwa akifanya vizuri kwa misimu kadhaa sasa, naye hivi sasa amekuwa akisababisha Msuva apate nafasi za kufunga. Naamini Yanga itachukua ubingwa kama Msuva atafunga walau mabao matano katika michezo saba iliyosalia, lakini anaweza asifunge idadi hiyo ya mabao nab ado mchango wake ukafanikisha kupatikana kwa mabao hayo, licha ya kuwa yeye ni kiungo alisi wa pembeni.
Kwa sasa tunamuona mchezaji ' namba 10 wa uongo' ambaye ataendelea kufanya kufunga mabao kwa kuwa hata yeye anafahamu yuko katika kiwango cha juu. Huku akiwa ameshabeba taji moja la ligi kuu tangu alipojiunga na Yanga miaka miwili na nusu iliyopita, Msuva amekuwa mchezaji muhimu zaidi msimu huu katika ufungaji wa mabao katika kikosi cha Yanga, huku wakijiweka sawa kuhakikisha wanarudisha ubingwa wa Bara ' Mitaa ya Twiga na Jangwani' mchezaji huyo anastahili kupewa tuzo ya heshima; Kama mchezaji bora wa klabu msimu huu.
Huenda asipewe sifa anazostahili, lakini Msuva yuko katika kiwango ambacho anastahili kushinda hata tuzo moja ya mchezaji bora wa mwezi katika ligi kuu msimu huu. Kiwango chake hakitaishia hapo hadi atakapovaa medali nyingine ya ligi kuu Tanzania Bara. Kwa sasa ndiye mchezaji anayebadilisha mbinu za mashambulizi za Yanga ni Msuva. Kwa maana kwana uwezo wake wa kucheza kama kiungo ' asilia namba-7',
Labda sasa huu ni wakati na Msuva, na pengine apewe jezi namba 7 ya Taifa Stars sasa tupate huduma yake. Kijana anatisha kama ' kimeta', mimi nampongeza Msuva kwa jitihada zake, uvumilivu wake, ubora wake wa uwanjani. Bila shaka anakuja kuwa dili kubwa sokoni wakati wa usajili ujao. Kama unataka ufalme, tulia sehemu moja. Kwa sasa Msuva anapendeza kuichezea Yanga. Kinara wa mabao ligi kuu Tanzania Bara, 11 goals….Bado ana safari ndefu….Tunaisema zaidi Yanga kwa vile tunaona.. Hapana njia moja pekee ya kufikia mafanikio kama ' Uvumilivu na Jitihada'
0714 08 43 08
Comments
Post a Comment